Naomba wasanii wakongwe tuache kuwa-diss hawa watoto – Dudu Baya
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Tanzania, Dudubaya amewachana wasanii wenzake wakongwe kuacha tabia za kuwa-diss wasanii wadogo kwenye game ambao wanafanya vizuri kwa sasa na badala yake wajikite kutengeneza ngoma kali ili waweze kurudisha heshima yao.

Dudu Baya
Dudu Baya amesema wasanii wakongwe wanapaswa kujitengenezea brand yao ili waweze kuendelea kuwepo kwenye ‘game’ huku akiongeza kwamba kama kazi zikifanyika vizuri wanaweza kurudi katika nafasi zao.
“Mi ningeomba wasanii wakongwe tuache kuwa-diss hawa watoto wanaofanya vizuri katika game, cha kwanza tutambue siyo lazima kila siku tuonekane sisi tu, ndio maana tunapata watoto wa kuturithi. Lakini utakuta baadhi ya wasanii wakongwe wamekaa pamoja wanakula bangi hata sabini wanalalamikia watoto wanaojitafutia rizki zao, nawaambia mtakufa” , amesema Dudubaya kwenye mahojiano yake na East Africa Radio.
Dudu Baya ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya ‘Inuka’ aliyomshirikisha TID, ni moja ya wasanii wakongwe waliouanza mwaka vizuri na tutegemee kumuona akirudi kwa kasi kwenye game.
Post a Comment