Ongezeko la joto lapelekea wafanyakazi kupewa likizo
Waziri mkuu nchini Iraq, Haider al-Abadi ameamuru wafanyakazi wote wa Serikali kuchukua likizo kwa muda kutokana na kupanda kwa viwango vya joto nchini humo.

Watabiri wa hali ya hewa nchini humo wametabiri ongezeko la viwango vya joto kwenye mji mkuu, Baghdad kuwa leo ijumaa Agosti 11 kutakuwa na joto la kiwango cha juu kati ya 40 Celsius – 50 Celsius.
Maeneo mengine yatakayoathiriwa zaidi na joto ni miji ya Basra na Mosul, mbali na mathara yatayojitokeza kiafya pia kuna uwezekano kukosekana kwa umeme kuanzia leo.
Viwango vya juu vya joto vinakadiriwa kuongezeka duniani na tayari vimeanza kuathiri maeneo ya bara la Ulaya na maeneo mengine ya Asia.
Wanasayansi wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha vifo vya watu 52,000 barani Ulaya mwaka 2100 ikiwa hatua madhubuti hazitafanyika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa
Post a Comment